Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

MAMBO MANNE YA NGUVU YA KUJIFUNZA NANENANE 2026

Imewekwa: 16 Sep, 2026
MAMBO MANNE YA NGUVU YA KUJIFUNZA NANENANE 2026

Ujumbe wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD) umekutana na Wizara ya Kilimo kujadili Tathmini ya Muda wa Kati (Mid-Term Review) ya Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) unaotekelezwa na Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano na Shirika hilo.

Kikao kimefanyika tarehe 01 Septemba 2026, jijini Dodoma ambapo Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la IFAD Tanzania, Bw. Sakphouseth Meng amezungumza na Kaimu Katibu Mkuu, Mhandisi Athumani Kilundumya kuhusu matokeo ya Programu hiyo na kuweka mipango madhubuti kwa kipindi kilichobaki cha mwaka mmoja na miezi sita.

Mha. Kilundumya amesema kuwa Programu ya AFFP imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya mbegu, miundombinu, mafunzo kwa wakulima pamoja na wasambazaji wa pembejeo, ambapo takribani wasambaji wa pembejeo 800 wamepata elimu ya matumizi sahihi ya mbegu bora.

Mafanikio haya yameongeza uzalishaji wa mbegu kwa kufikia asilimia 68 ya lengo la kuzalisha tani 13,000 ya mbegu bora akitolea mfano katika shamba la mbegu la Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), lilipo Kilimi Nzega ambalo asilimia 90 ya miundombinu yake imejengwa kupitia programu hiyo.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao, Dkt. Yasinta Nzogela; wakiwemo Mratibu wa AFDP; Wawakilishi kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA); Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI); Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI); Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI).