Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

MWELI AFANYA ZIARA BELARUS KUIMARISHA MAGEUZI YA SEKTA YA KILIMO

Imewekwa: 03 Jun, 2026
MWELI AFANYA ZIARA BELARUS KUIMARISHA MAGEUZI YA SEKTA YA KILIMO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli amemwakilisha Mhe. Daniel Chongolo (Mb), Waziri wa Kilimo katika ziara ya kikazi nchini Belarus ambapo amepokelewa na Mhe. Vitali Kulak, Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula wa Jamhuri ya Belarus.

Katibu Mkuu anatarajiwa kutembelea kampuni mbalimbali zinazotengeneza matreka; kampuni zinazotengeneza teknolojia za uhifadhi wa mazao baada ya kuvunwa; kampuni za utengenezaji wa magari ya kusafirishia mazao na chakula.  

Vile vile, Katibu Mkuu Mweli atatembelea maonesho ya kilimo ya Belarus kupata uzoefu zaidi wa teknolojia na bidhaa zinazooneshwa; atatembelea mashamba ya uzalishaji ngano; zikiwemo Taasisi za Utafiti za nchi hiyo ili kupata ujuzi na uzoefu utakaosaidia kufanya mageuzi katika Sekta ya Kilimo hapa na kutekeleza malengo ya DIRA 2050.

Akiwa nchini Belarus, Katibu Mkuu Mweli pia anatarajiwa kukutana kwa mazungumzo na Waziri wa Viwanda na Waziri wa Kilimo na Chakula.