WAKULIMA ZAIDI YA 1000 KATIKA VIJIJI VYA SUNGWIZI, NKINGA NA SIMBO WAIPONGEZA SERIKALI KWA ELIMU YA MBOLEA NA MBEGU
Wakulima zaidi ya 1000 katika vijiji vya Sungwizi, Nkinga na Simbo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora waipongeza Serikali kwa kuwafikia na kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mbolea na mbegu bora ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao wanayolima.
Wakulima hao wamepatiwa mafunzo kwa nyakati tofauti kuanzia tarehe 5 hadi 7 Desemba 2025 kutoka kwa wataalamu wa Wizara ya Kilimo wakishirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kupitia Kampeni ya Mali Shambani
Igunga ni miongoni mwa maeneo yanayozalisha kwa wingi mazao ya Pamba, Choroko, Dengu, Mahindi, Karanga na Mpunga.