Skip to main content
Bodi za Mazao

Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB)

- Tanzania Tobacco Board (TTB)

Bodi ya Tumbaku Tanzania ni chombo cha udhibiti wa zao la tumbaku kilichoanzishwa chini ya sheria ya sekta ya  tumbaku Na. 24 ya 2001 (kama ilivyorekebishwa na sheria ya mazao (marekebisho mchanganyiko) Na. 20 ya 2009). 

Historia ya Bodi ya Tumbaku inakwenda nyuma katika miaka ya 1960 wakati wa iliyokuwa Bodi ya Tumbaku Tanganyika.  Katika mwaka 1970 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianzisha Mamlaka ya Tumbaku Tanzania (TAT).  TAT ilibadilishwa mwaka 1984 na kuwa Bodi ya Usindikaji wa Tumbaku na Masoko Tanzania (TTP & MB).  

Mwaka 1993 TTP & MB ilifanyiwa marekebisho na kuwa Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) kufuatia ubinafsishaji wa sehemu ya sekta ya tumbaku ambayo ulifikia kilele chake mwaka 1997 wakati shughuli za kibiashara za TTB zilipo kasimiwa kwa ujumla wake kwa sekta binafsi. TTB ya sasa imekuja baada ya kuidhinishwa kwa sheria ya sekta ya tumbaku Na. 24 ya 2001. Kwa mujibu wa sheria ya sekta ya tumbaku Na.24 (2001) na marekebisho yake (2009), TTB ina mamlaka maalum yafuatayo kwa ajili ya sekta ndogo ya tumbaku:-

  • Kusajili au kutoa leseni kwa wakulima , wauzaji na wasindikaji wa tumbaku,
  • Kutoa leseni kwa wanunuzi, wauzaji na wasindikaji wa tumbaku,
  • Kutoa leseni kwa ajili ya kusafirisha au uingizaji wa tumbaku kutoka au katika Tanzania
  • Kuteua wakaguzi kwa ukaguzi wa maeneo ya tumbaku, na kitu kingine chochote ambacho kinaweza kukaguliwa kwa ajili ya utekelezaji bora wa masharti ya sheria.

BODI YA TUMBAKU TANZANIA
Mtaa wa Bima, Ploti Na. 375 Kitalu 'B' Kihonda,
Jengo la Tumbaku, Ghorofa ya chini,
P.O. Box 227, Morogoro, Tanzania.
Namba ya Simu: 023-26030364/2604517
Namba ya Nukushi: 023-2604401
Barua pepe: info@tobaccoboard.go.tz

https://www.tobaccoboard.go.tz/