Skip to main content
Taasisi za Wizara

Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF)

Mfuko wa Pembejeo ni taasisi ya Serikali inayotoa mikopo ya Pembejeo za Kilimo/Mifugo na Zana za Kilimo. Mikopo inayotolewa na Mfuko wa Pembejeo ninkwa ajili ya kupanua maeneo ya kilimo na kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi. Muda wa mikopo ni kati ya miaka miwili (2) hadi mitano(5) kutegemea aina ya mkopo. Riba ya mkopo ni asilimia sita (6%) hadi nane (8%) kutegemea aina ya mkopo.

Dhamana za mikopo ni hatimiliki au leseni ya makazi ya mali isiyohamishika kwa waombaji binafsi kampuni. Kwa Vyama vya Ushirika na Taasisi za Kijamii zisizo na dhamana zenye hati miliki au leseni za makazi za mali zisizohamishika, dhamana ni akiba za wanachama (30%) na Halmashauri husika (70%). Fomu za maombi ya mikopo zinapatikana kwenye tovuti hii, Ofisi za Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Jiji. Mkopo utaanza kurejeshwa baada ya mwezi mmoja hadi sita. Fedha ya Mkopo italipwa kwenye Kampuni ya chaguo la mwombaji.

WALENGWA WA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA PEMBEJEO

  1. Walengwa ni;
  2. Wakulima binafsi.
  3. Makampuni.
  4. Vikundi na Taasis i za Kijamii zilizosajiliwa na zinazojishughulisha na Kilimo.
  5. Wasambazaji wa pembejeo za kilimo,mifugo na Uvuvi.
  6. Wenye viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya Kilimo,mifugo na uvuvi.

DIRA

Kuwa kinara chaguo katika kutoa mikopo ya Pembejeo na zana kwa riba nafuu kwa wakulima/wafugaji na wavuvi wadodo katika kuitikia wito na mahitaji ya maendeleo ya Kilimo Tanzania.

Kutoa mikopo ya riba nafuu kwa wakulima,wafugaji na wavuvi wadogo nchini Tanzania ili kuboresha maisha ya kaya pamoja na usalama wa chakula wa Taifa.

DHAMIRA

Kwa kuwakopesha wakulima moja kwa moja, mawakala wa usambazaji wa pembejeo nchini, vyama vya msingi vya wakulima ama mawakala wao, SACCOS kuwajengea uwezo wa kusimamia shughuli za kilimo kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya, Miji na Manispaa, Sekta binafsi na wadau wengine kwa maendeleo ya kilimo.

Kupanua maeneo ya Kilimo na kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi.

Pakua Faili:

https://www.agitf.go.tz/