Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

BENKI YA USHIRIKA TANZANIA KULETA MATUMAINI KWA WAKULIMA WA DODOMA

Imewekwa: 26 Apr, 2025
BENKI YA USHIRIKA TANZANIA KULETA MATUMAINI KWA WAKULIMA WA DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule amefanya mkutano na waandishi wa habari tarehe 25 Aprili 2025 na kuhamasisha wakazi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa ya jirani kushiriki katika Uzinduzi wa Benki ya Ushirika Tanzania (COOP Bank Tanzania).

Mkutano huo ulimshirikisha pia Bw. Godfrey Ng’urah, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ushirika. 

Benki hiyo inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 28 Aprili 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.