Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

CHONGOLO AHIMIZA UBUNIFU NA UTENDAJI WA KAZI KWA UFANISI KWA TAASISI ZA WIZARA YA KILIMO

Imewekwa: 14 Apr, 2026
CHONGOLO AHIMIZA UBUNIFU NA UTENDAJI WA KAZI KWA UFANISI KWA TAASISI ZA WIZARA YA KILIMO

Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb) amefanya kikao kazi na Wakurugenzi Wakuu na Wenyeviti wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara:  Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI); Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB); Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Mbegu Tanzania (TOSCI); na Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), kujadili utekelezaji wa mikakati mbalimbali waliyojiwekea kwa mwaka wa fedha 2025/2026 pamoja na kuangalia mwelekeo wa mikakati ya mwaka ujao wa fedha 2026/2027.

Waziri Chongolo  amesisitiza umuhimu wa Taasisi hizo kufanya kazi kwa ufanisi na ubunifu ili kuhakikisha Sekta ya Kilimo inaendelea kuwa mhimili mkuu wa uchumi wa Taifa, huku akitaka kuimarishwa kwa uratibu, uwajibikaji na matumizi ya teknolojia ili kuongeza tija na ushindani kwa manufaa ya wakulima na Taifa kwa ujumla.

Kikao hicho pia kimeshirikisha Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb); Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Umwagiliaji na Zana za Kilimo, Mha. Athuman Kilundumya; Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Prof. Peter Msoffe; pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Kilimo.