Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

CHONGOLO AITAKA ASA KUZALISHA MBEGU KWA TIJA

Imewekwa: 02 Nov, 2026
CHONGOLO AITAKA ASA KUZALISHA MBEGU KWA TIJA

Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb) amewataka watumishi wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kufanya kazi yenye tija inayoonekana, marina na ubunifu ili kuleta matoneo kwa wananchi. Akiwa ziarani mkoani Tabora, Mhe. Chongolo amesema kuwa shamba la mbegu la Kilimi ni miongoni mwa mashamba yanayomilikiwa na ASA yenye jukumu la kuweka msukumo wa uzalishaji wa mbegu nchini ili kupunguza utegemezi wa mbegu kutoka nje ya nchi.  Aidha, Waziri Chongolo ameielekeza ASA kuongeza uwekezaji wa miundombinu ya umwagiliaji, ili kuhakikisha msimu ujao uzalishaji unaongezeka kwa kiwango kikubwa zaidi. (Oktoba 2026)