COPRA YASAINI MAKUBALIANO NA TAASISI YA CORUS INTERNATIONAL KUKUZA ZAO LA KAKAO
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) ameshiriki katika hafla ya utiaji sahini wa makubaliano kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) na Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi (CORUS) kwa ajili ya kuongeza uzalishaji na kukuza soko la kimataifa la mazao ya kakao na kahawa nchini tarehe 25 Aprili 2025, katika hoteli ya Zabibu jijini Dodoma.
Naibu Waziri Silinde amesema ushirikiano huo utaongeza tija na uzalishaj kwa wakulima, kuongezeka kwa wigo wa masoko mapya kwa kubidhaisha mazao ili yawe na viwango vya masoko ya kimataifa.
Naye Mkurugenzi wa COPRA, Bi. Irene Mlola amesema kuwa sehemu ya makubaliano hayo ni kuhakikisha wakulima wanalima kilimo endelevu chenye kuzingatia taratibu bora za kilimo, kuongeza tija na uzalishaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Aidha, Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa amesema makubaliano hayo pia yataongeza ubora wa zao la Kahawa, kupanua masoko, kuongeza kipato cha mkulima na kuwa na mazingira bora na wezeshi ya biashara.