Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

UJUMBE WA IFAD WAIPONGEZA WIZARA YA KILIMO

Imewekwa: 02 Nov, 2026
UJUMBE WA IFAD WAIPONGEZA WIZARA YA KILIMO

Ujumbe wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD) umeipongeza Wizara ya Kilimo kufuatia zoezi la Tathmini ya Muda wa Kati (Mid-Term Review) ya utekelezaji wa programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP).

Kikao kimefanyika tarehe 01 Septemba 2026 jijini Dodoma, ambapo Mkurugenzi Mkazi wa IFAD Tanzania, Bw. Sakphouseth Meng amezungumza na Kaimu Katibu Mkuu, Mhandisi Athumani Kilundumya kuhusu matokeo ya programu hiyo ambayo imekuwa mchango mkubwa katika maendeleo ya mbegu, miundombinu, mafunzo kwa wakulima pamoja na wasambazaji wa pembejeo 800 waliopata elimu ya matumizi sahihi ya mbegu bora.  

Mafanikio yameongeza uzalishaji wa mbegu kwa kufikia asilimia 68 ya lengo la kuzalisha tani 13,000 ya mbegu bora akitolea mfano katika shamba la mbegu la Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) lililopo Kilimi, Nzega ambalo asilimia 90 ya miundombinu yake imejengwa kupitia programu hiyo.