Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

MFUMO WA USAJILI WA JUKWAA LA HOTIKACHA LA KIMATAIFA WAZINDULIWA

Imewekwa: 23 Apr, 2026
MFUMO WA USAJILI WA JUKWAA LA HOTIKACHA LA KIMATAIFA WAZINDULIWA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amezindua rasmi mfumo wa usajili kuelekea Jukwaa la Hotikacha la Kimataifa (HortiLogistica Africa 2026) tarehe 22 Aprili 2026, jijini Dodoma.

Jukwaa hilo la wazalishaji wa mazao na Wadau wa mnyororo mzima wa hotikacha linalenga kukutanisha wawekezaji, wasindikaji, wachakataji, wakulima wafanyabiashara na Wadau wengine Muhimu zaidi 15,000 jijini Arusha, tarehe 8 hadi 10 Novemba 2026.  Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Mkuu Nchemba amesema kuwa mwana-mageuzi Kiongozi katoka sekta ya chakula na nyingine Mhe. Rais Dkt. Samia ametoa salamu zake na pongezi kufuatia tukio hilo muhimu na la kihistlria litakalochochea uwekezaji, biashara na masoko ndani na nje ya nchi.

Waziri Mkuu Nchemba amesema Jukwaa la Hotikacha la Kimataifa (HortiLogistica Africa 2026) litakuwa pia dirisha la guess kwa kizazi cha na cha baadaye, huku akisisitiza wananchi kuchangamkia fursa hiyo ambayo ina zaidi ya wakulima milioni 10 kwenye mazao ya hotikacha.  Ametoa rai kwa wakulima kuzingatia ubora na viwango vya mazao wanayozalisha ili kuongeza wigo wa masoko katika Jukwaa hilo limalotarajiwa luganyika mwezi Novemba 2026. 

Viongozi walioshiriki uzinduzi ni pamoja Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la Kukuza Kilimo na Kuongeza Uzalishaji wa Chakula; Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo; Mhe. Daniel Chongolo (Mb), Waziri wa Kilimo; Mhe. David Silinde (Mb), Naibu Waziri wa Kilimo; Bw. Gerald Mweli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo; Mha. Athumani Kilundumya, Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Umwagiliaji na Zana za Kilimo. Wengine ni Dkt. Jacqueline Mkindi, Mkurugenzi Mtendaji wa TAHA na Bi. Irene Mlola, Mkurugenzi Mkuu wa COPRA.