Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb), amekutana na Balozi wa Ufalme wa Saudi Arabia nchini Tanzania
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb), amekutana na Balozi wa Ufalme wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Mhe. Yahya Okeish, na kufanya naye mazungumzo kabla ya kushiriki katika hafla ya makabidhiano ya awamu ya kwanza ya Mradi wa Uzalishaji wa Zao la Tende unaoshirikisha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO). Viongozi hao wamekutana tarehe 15 Septemba 2026, katika ofisi iliyopo ndani ya Maabara Kuu ya TARI, Mtumba, jijini Dodoma.
Wengine katika picha ni Dkt. Yasinta Nzogela, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao, Wizara ya Kilimo; Dkt. Thomas Bwana, Mkurugenzi Mkuu wa TARI; pamoja na Bw. Abdullah Zahyan, Meneja wa KSRelief Programu ya Maendeleo ya Zao la Tende na wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.