Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

PROGRAMU YA BBT YAHIMIZWA KULETA MATOKEO YA HARAKA KWA VIJANA

Imewekwa: 17 Dec, 2025
PROGRAMU YA BBT YAHIMIZWA KULETA MATOKEO YA HARAKA KWA VIJANA

Programu ya vijana ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT Program) imehimizwa kuleta matokeo ya haraka kwa vijana kama vile kutafuta miradi ya mazao ya muda mfupi ili tija ipatikane kwa vijana kwa kutekeleza miradi yenye tija na kipato cha uhakika.

Akiongea na mratibu wa programu ya BBT katika kikao cha Menejimenti ya Wizara tarehe 15 Desemba 2025, Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb) amesema kuwa programu hiyo Inapaswa kuongeza ubunifu endelevu na kuongeza kasi ya ushiriki wa vijana katika kilimo.  “Lazima kila Kiongozi ndani ya Wizara awe na shamba analolisimamia kwa lengo la kutoa hamasa na ushiriki katika shughuli za kilimo,” ameeleza Waziri Chongolo. 

Kwa kuzingatia utaratibu huo, Waziri Chongolo anehimiza BBT programu kuwapangia viongozi wa Wizara kila mmoja wao mashamba mawili ya BBT ambapo viongozi hao watasimamia na kufuatilia watafuatilia kwa karibu.

Katika hatua nyingine, Waziri Chongolo ameelekeza miradi inayotekelezwa ni Wizara ambayo ni Programu ya Mifumo Himilivu ya Chakula Nchini (TFSRP); Mradi wa Kuwezesha Upatikanaji wa Pembejeo za Kilimo Tanzania (TAISP) na Programu ya BBT kuimarisha ushirikiano kwa kuweka mikakati ya pamoja yenye mwelekeo wa kuongeza kasi ya ukuaji wa  Sekta ya Kilimo. 

Vile vile, Waziri Chongolo amefanya kikao na Menejimenti na Wakuu wa Taasisi za Wizara ya Kilimo na kutoa msisitizo wa kuongeza jitihada za utekelezaji malengo yaliyodhamiriwa kupitia Agenda 10/30 na Mpango Kabambe wa Mageuzi ya Sekta ya Kilimo 2050 (Agricultural Master Plan 2050) na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.