RAIS SAMIA AWAPA MATUMAINI WAKULIMA WA PAMBA

“Tunataka tuipandishe Pamba kama tulivyofanya kuwafaidisha kwenye mazao mengine ili wakulima walime kwa faida ya uchumi wao. Tunataka Pamba yetu tuitengeneze hapa hapa nchini,” amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akiongea na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu tarehe 16 Juni 2025.
Amesema uwekezaji wa ndani wa Kiwanda cha Moli Oil Mills Ltd. umefungua fursa za ajira, na hivyo Serikali haina budi kuongeza uwekezaji katika utengenezaji wa nyuzi za Pamba hapa nchini.
Kiwanda hicho cha Moli Oil Mills Ltd. kimezinduliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia ambapo aliweka jiwe la msingi na kukata utepe mbele ya mamia ya wananchi na wakazi wa Mkoa wa Simiyu wameshuhudia uzinduzi huo.
Katika ziara hiyo, Mhe. Rais Dkt. Samia pia amezindua Kiwanda cha kutengeneza Mabomba ya maji cha kampuni ya Moli Oil Mills Ltd.
Vilevile, Mhe. Rais amezindua Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
Viongozi wa Serikali waliombatana na Mhe.Rais Dkt. Samia katika ziara yake ni pamoja na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli.