Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

TANZANIA NA KENYA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA KILIMO

Imewekwa: 21 May, 2026
TANZANIA NA KENYA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA KILIMO

Tanzania na Kenya zaahidi kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika Sekta ya Kilimo hususan katika nyanja za kukuza biashara, uwekezaji pamoja na kuimarisha usalama wa chakula ukanda wa Afrika Mashariki.

Hayo yamebainishwa wakati wa majadiliano kati ya Bw. Gerald Mweli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mhe. Catherine Wahome, Balozi wa Jamhuri ya Kenya nchini Tanzania tarehe 20 Mei 2026,
Mtumba - jijini Dodoma. 

Katibu Mkuu Mweli ameeleza utayari wa Tanzania kushirikiana na Kenya katima Sta ya Kilimo, huku akigusia  Hati ya Makubaliano (MoU) baima ya nchi Hizo mbili iliyosainiwa hivi karibuni tarehe 04 Mei, 2026 jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya kiserikali ya Mheshimiwa Dkt. William Ruto, Rais wa Jamhuri ya Kenya.  Utekelezaji wa hati hiyo unahusisha timu ya wataalam kutoka pande zote mbili kwa ajili ya kuratibu utekelezaji wa makubaliano hayo pamoja na kuandaa mpango kazi wa pamoja.

Hati hiyo ilisainiwa na Mawaziri wenye dhamana ya Kilimo wa nchi husika ambao ni Mhe. Daniel Chongolo (Mb), Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Seneta Mutahi Kagwe EGH, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo wa Jamhuri ya Kenya.  

Viongozi hao pia wamejadili kuhusu umuhimu wa kuoanisha masharti ya vyeti vya usafi wa mimea ili kuondoa vikwazo visivyo vya kikodi katika biashara ya mazao ya kilimo, na hivyo kuongeza biashara ya mazao kati ya Tanzania na Kenya.