Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

TANZANIA NA MALAWI ZASAINI TAMKO LA PAMOJA LA KIBIASHARA; BIASHARA KUENDELEA KAMA ILIVYOKUWA AWALI

Imewekwa: 02 May, 2025
TANZANIA NA MALAWI ZASAINI TAMKO LA PAMOJA LA KIBIASHARA; BIASHARA KUENDELEA KAMA ILIVYOKUWA AWALI

Tanzania na Malawi zimekubaliana kuendelea na biashara kuanzia tarehe 02 Mei, 2025.

Tamko la Pamoja (Joint Communiqué) limesainiwa tarehe 2 Mei 2025 kufuatia kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje; Kilimo; Viwanda na Biashara wa pande zote jijini Dodoma.

Kusainiwa kwa Tamko la Pamoja ni uthibitisho wa kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Malawi kwa bidhaa mbalimbali ikiwemo mazao ya kilimo kulingana Mikataba na miongozo ya Kikanda na Kimataifa iliyopo.