Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

WIZARA YA KILIMO KUIMARISHA USHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA YANAYOHUSIKA NA SEKTA YA KILIMO

Imewekwa: 07 Feb, 2026
WIZARA YA KILIMO KUIMARISHA USHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA YANAYOHUSIKA NA SEKTA YA KILIMO

Mhe. Daniel G. Chongolo (Mb.), Waziri wa Kilimo amefanya kikao na Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italia na Mwakilishi wa Kudumu kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa FAO, IFAD na WFP, tarehe 3 Februari 2026 jijini Dar es Salaam. 

Kikao hicho kimefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Afrika kuhusu Matumizi Endelevu ya Zana za Kilimo (Africa Conference on Sustainable Agricultural Mechanization – ACSAM) unaofanyika kuanzia tarehe 3-6 Februari 2026. 

Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wamekubaliana kukuza diplomasia ya uchumi katika Sekta ya Kilimo hususan katika kuiwezesha dawati la Ubalozi nchini Italian linaloratibu shughuli za mashirika ya Kimataifa yanayohusika na Sekta ya Kilimo.