Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

ZOEZI LA UPIMAJI AFYA YA UDONGO KANDA YA ZIWA

Imewekwa: 14 Oct, 2025
ZOEZI LA UPIMAJI AFYA YA UDONGO KANDA YA ZIWA

Wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo wameanza zoezi la upimaji wa Afya ya Udongo tarehe 13 Ocktoba, 2025 katika Mikoa ya Mwanza, Geita na Simiyu.

Zoezi hilo litaambatana na uchimbaji wa mashimo makubwa (soil profile) na uchukuaji wa majira nukta (sample point) katika maeneo mbalimbali kulingana na usomaji wa ramani ya eneo husika.

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Kilimo, Mha. Juma Mdeke amesema timu za kukusanya sampuli  za udongo  kwa ajili ya kufanya uchakataji zipo uwandani katika mikoa ya Kanda ya Ziwa Mwanza, Simyu na Geita.

Amefafanua zaidi kuwa zoezi hilo linatarajiwa kukusanya zaidi ya sampuli 1000 ambazo zitapelekwa maabara kwa ajili ya uchakataji ili kupata taarifa zaidi kuhusu afya ya udongo  ya eneo; rutuba; aina ya mazao yanayotakiwa kulimwa kwenye maeneo hayo na pia kupata taarifa kuhusu aina za mbolea na kiasi cha mbolea kinachotakiwa kwa ajili ya kilimo katika eneo husika.  

Zoezi hilo limelenga kuwa na ramani ya afya ya udongo, mazao yanayotakiwa kulimwa katika eneo husika ili kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji kwenye Mikoa hiyo