Skip to main content
Taarifa
Kiingereza

TAARIFA YA WIKI YA MWENENDO WA BEI ZA MAZAO YA CHAKULA 07 - 11 Juni, 2021

Wastani wa bei kitaifa umebadilika kwa viwango tofauti tofauti. Bei za mahindi, maharage, mtama, na viazi mviringo zimepungua kwa asilimia 3, 2, 1 na 1 mtawali. Bie ya mchele haijabadilika.

Mboga na Matunda (Horticulture): Bei katika masoko mbalimbali nchini zimebadilika kwa viwango tofauti. Bei za nanasi, na vitunguu zimeongezeka kwa asilimia 1, wakati bei za tikiti maji, pilipili hoho na tango, zimepungua kwa asilimia 5, 3 na 2 mtawalia.

Tumbaku: Hadi kufikia tarehe 06 June, 2021 kiasi cha tumbaku kilichouzwa ni Kilo 19,305,139 zenye thamani ya Dola za Kimarekeni za 29,043,525. ✓ Kahawa: Hadi kufikia tarehe 27 Mei, 2021 kahawa iliyouzwa kwa msimu wa mauzo 2020/21 ni tani 70,043 zenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 137.6.

Ufuta: Hadi kufikia tarehe 5 Juni, 2021 ufuta uliouzwa kwa msimu wa mauzo 2021/22 ni tani 5,099.