Skip to main content
Taarifa
Kiingereza

TAARIFA YA WIKI YA MWENENDO WA BEI ZA MAZAO YA CHAKULA 21 - 25 Juni, 2021

Ujumbe Wastani wa bei kitaifa umebadilika kwa viwango tofauti tofauti. Bei za mahindi na mchele zimeongezeka kwa asilimia 2, bei za maharage hazijabadilika, wakati bei mtama na viazi mviringo zimepungua kwa asilimia 4.

Mboga na Matunda (Horticulture): Bei katika masoko mbalimbali nchini zimebadilika kwa viwango tofauti. Bei za nanasi, na vitunguu zimeongezeka kwa asilimia 1, wakati bei za tikiti maji, pilipili hoho na tango, zimepungua kwa asilimia 5, 3 na 2 mtawalia.

Tumbaku: Hadi kufikia tarehe 20 Juni, 2021 kiasi cha tumbaku kilichouzwa ni Kilo 29,122,687 zenye thamani ya Dola za Kimarekeni za 44,633,382.

Pakua Faili: