Skip to main content
Ripoti
Taarifa
Swahili

Taarifa ya Tathmini ya Kina ya Hali ya Usalama wa Chakula na Lishe Nchini

ilizingatia mihimili minne ya usalama wa chakula ambayo ni  Upatikanaji (Food availability), Ufikiwaji wa Chakula (Food accessibility), Utumiaji na Ulaji wa Vyakula (Food Utilization) na Uendelevu wa uhakika wa chakula (Stability). Taarifa nyingine  zilihusu masuala ya hali ya hewa (hususan mvua kwa ustawi wa mimea); majanga yaliyopo sasa na yale yanayoweza kujitokeza na kuathiri usalama wa chakula na lishe, njia mbadala wanazotumia wananchi kukabiliana na matatizo ya chakula na lishe kwa sasa. Pia, masuala ya usafi na maji ikiwa ni kati ya vigezo vinavyoweza kuathiri usalama wa chakula na lishe ni sehemu ya taarifa zilizokusanywa, kuchambuliwa na kutolewa taarifa.  

Taarifa zote zilizokusanywa na kuchambuliwa zilijumuishwa ili kupata picha halisi ya masuala ya usalama wa chakula na lishe kwa mapana yake katika maeneo hayo. Nyenzo ya Mfumo wa kunyumbulisha na kuainisha madaraja (Phases) ya jamii/watu ngazi ya kaya na maeneo kulingana na hali zao za Usalama wa Chakula na Lishe -(Intergrated Food Security Phase Classification-IPC) ilitumika kuwezesha uchambuzi wa takwimu hizo. Nyenzo  ya IPC inatafasiri hali ya usalama na lishe katika madaraja (phases) matano kulingana na kiwango cha athari katika usalama wa chakula. 

Aidha IPC imebainisha na kupendekeza aina ya hafua inayohitajika kulingana na daraja/kundi. Aidha, kwa kutumia IPC na kuzingatia mchanganuo wa vigezo mbalimbali tathmini imebainisha hali halisi ilivyo kuanzia Novemba, 2019 hadi Aprili, 2020  kabla ya mavuno ya msimu wa 2019/20  (Current situation Analysis) na hali tarajiwa katika kipindi cha mwezi Mei hadi Septemba 2020 (Projected situation Analysis) baada ya mavuno ya msimu wa 2019/20.

Pakua Faili: