Wizara ya Kilimo kupitia Programu ya Mifumo Himilivu ya Chakula (TFSRP) imekabidhi vifaa vya kisasa vya umwagiliaji kwa vikundi vitatu vyenye jumla ya wakulima 94 wa mazao ya bustani, matunda na mazao mengine ya chakula katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza, tarehe 10 Novemba 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli akizungumza na Waandishi wa Habari tarehe 6 Novemba 2025, jijini Dodoma kuhusu mkutano mkubwa wa wadau wa mazao ya mboga na matunda utakaowakutanisha washiriki kutoka ndani na nje ya nchi, kwa lengo la kujadili fursa, changamoto na mikakati ya kukuza Sekta hiyo.
Mkutano huo utafanyika tarehe 12 - 13 Novemba 2025 jijini Dar es Salaam, ukiwa ni wa kwanza wa aina yake nchini, na utaendelea kufanyika kila mwaka.