Skip to main content
Habari na Matukio

BASHE ASISITIZA MSHIKAMANO KWA WATUMISHI WA WIZARA YA KILIMO

Waziri wa Kilimo Mhe Husein Bashe, amefungua kikao Cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo jijini Dodoma.

Kikao hicho kilihudhuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli, Naibu Katibu Mkuu wa WizarayaKilimo Dkt
HusseinMohammedOmar,  Wakurugenzi wa Idara, Wakuu wa Vitengo, Viongozi wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), Wakuu wa Vyuo vya MATI pamoja na wawakilishi wa Wafanyakazi.

Waziri Bashe amewataka Wafanyakazi hao kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha Agenda 10/30 yenye lengo la kukuza sekta ya kilimo kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2030 inafanikiwa.

"Sisi  Watumishi wa Wizara  ya Kilimo tushikamane na kufanya kazi kwa kushirikiana, kila mtumishi lazima ajue kuwa kazi za idara zote zinamuhusu kwani ni  kazi za Wizara ; Mimi, Mhe.Naibu Waziri, Katibu Mkuu,Naibu Katibu Mkuu pamoja na Viongozi Wenzangu tutaendelea kuwa mfano wa mshikamano ili kuhakikisha tunatekeleza mipango na miradi yote ya maendeleo kwa mujibu wa  Bajeti" . Amesema Waziri Bashe