KATIBU MKUU MWELI AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA WIZARA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli amewakumbusha watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano, bidi na ufanisi ili kuleta tija katika Sekta ya Kilimo.
Katibu Mkuu Mweli ameyasema hayo katika mkutano wa Watumishi wa Wizara ya Kilimo uliofanyika jijini Dodoma tarehe 22 Februari jijini Dodoma.
Katika mkutano huo watumishi walipokea mawasilisho mbalimbali ya programu na miradi inayotekelezwa na ya Wizara Kilimo.
AIha Watumishi hao waliweza kupata mafunzu yanayohusu afya zao ikiwa ni pamoja na elimu ya kujilinda dhidi ya Virusi vya UKIMWI, Kifua Kikuu pamoja na na magonjwa yasiyoambukiza.
Katika kikao hicho Katibu Mkuu Mweli alisikiliza michango na maoni mbalimbali ya Watumishi na kutolea ufafanuzi na maelekezo ya utekelezaji wake kupitia Wakurugenzi na Wakuu Vitengo vilivyo chini ya Wizara ya Kilimo.
Mawasilisho yaliyowasilishwa ni ya utekelezaji wa Mradi wa Kusaidia Pembejeo za Kilimo Tanzania (TAISP), Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP); Programu ya Building a Better Tomorrow (BBT); na Programu ya Uvumilivu wa Mifumo ya Chakula Tanzania (TFSRP).