Skip to main content
Habari na Matukio

KITABU CHA KANUNI BORA ZA ZAO LA CHAI CHAZINDULIWA

Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe leo amezindua kitabu cha Kanuni Bora za Kilimo cha  Chai na Katibu cha Muongozo wa Mkulima wa Chai.

Mhe.Bashe amefanya uzinduzi huo kwenye maadhimisho ya Siku ya Chai Duniani ambayo kitaifa yamefanyika Jijini Dodoma.

Aidha  Waziri Bashe amezindua  Mfumo  utakaotumika kuingiza taarifa za Wakulima na Wadau wa mnyororo wa thamani katika zao la chai.

Waziri Bashe alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Chai Duniani ambayo kitaifa yalifanyika Jijini Dodoma.