Skip to main content
Habari na Matukio

Kutoka Bungeni

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) akiwa na baadhi ya Waheshimiwa Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara zingine wakijadiliana jambo kabla ya kujibu michango/hoja zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge katika ripoti zilizokaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa Fedha 2021/2022. 

Kamati Tatu zilizowasilishwa Bungeni, jijini Dodoma ni Taarifa ya Kamati za (LAAC) na (PAC) kuhusu hesabu zilizokaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC).