Skip to main content
Habari na Matukio

Picha za kongamano la 10 la wadau wa kilimo linaloendelea Dodoma

Matukio mbalimbali ya tarehe 18 Aprili 2024 ya mwendelezo wa Kongamano la Mwaka la Kujadili Mageuzi ya Sera za Mifumo ya Chakula, Uvuvi na Mifugo ambayo yamehusisha pia Viongozi wa Serikali akiwemo mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb). 

 

Kongamano hilo la siku 3 linaloendelea katika Ukumbi wa Mabeyo jijini Dodoma limekutanisha wadau mbalimbali wa kilimo  wa ndani na nje ya nchi; ambapo majadiliano mbalimbali yameendelea katika kutafakari miaka 10 ya mageuzi ya kisera na sheria nchini, kujadili mifumo, changamoto na kupendekeza maeneo ya kuimarisha sera, mifumo ya chakula himilivu, jumuishi na endelevu.