Skip to main content
Habari na Matukio

SERIKALI IMEPANGA KUJENGA VIWANDA VYA CHAI

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde (Mb) amesema serikali imepanga kujenga viwanda vitano kwa ajili ya wakulima wadogo wa chai ili kuwaondolea wakulima changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo kucheleweshewa malipo yao baada ya kuuza mazao yao.

Mhe. Silinde amezungumza hayo wakati akitoa shukrani kwa Kam Bunge ya Kudumu ya Viwanda Biashara, Kilimo na Mifugo iliyofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Ghala  la Kipawa  unatekelezwa na   Wakala wa Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania ( TSHTDA) jijini Dar es Salaam.

Mhe. Silinde amefafanua kuwa  viwanda hivyo vyote vitajengwa kwenye maeneo ambayo yana wakulima wa chai ili kuwapa unafuu wakuluma hao wa gharama za usafirishaji kutoka shambani kwenda viwandani pamoja na kuwaepusha wakulima na usumbufu wa kucheleweshewa malipo ya fedha zao baada ya kuuza chai.

 

Aidha  Kamati ya BunguE ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Kilimo na Mifugo na Uvuvi   imeiopongeza Wizara ya Kilimo kwa  utekelezaji wa mradi huo  ambao umezingatia viwango vya ubora.

Akizungumza   baada ya ukaguzi wa mradi huo Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Deo Mwanyika amesma kamati imefurahishwa na viwango vya utekelezaji wa mradi huo.

Mhe. Mwanyika ameipongeza Wizara ya Kilimo kwa kuanzisha mnada wa chai hapa nchini ambao hapo awali ulikuwa ukiendeshwa nchi jirani.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo  Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania (TSHDA)  Bw. Theophord Ndunguru amesema mradi huo ulianzishwa kama kitega Uchumi cha Wakala lakini baada ya TSHTDA kuunganishwa na  Bodi ya Chai, jengo hilo litatumika kwa ajili yam nada wa chai.

Mkurugenzi Ndunguru amesema gharama za mradi huo ni 743,854,516 ambapo hadi sasa kiasi kilicholipwa ni  716,978,974.

Aidha Bw. Ndunguru amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha za mradi huo kwa wakati.