Skip to main content
Habari na Matukio

SERIKALI KUJENGA KONGANI YA VIWANDA VYA KOROSHO NA UFUTA  KUSINI  _(INDUSTRIAL PARK)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza Mpango wa Serikali wa Kujenga *_ Industrial Park_ * eneo la Maranje Nanyamba Kwa ajili ya uchakataji wa mazao ya korosho na ufuta. 

Mhe. Rais Samia Amesema hayo leo tarehe 15 Septemba 2023 wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara.

Kiwanda hicho cha uchakataji wa korosho na zao la ufuta kitafikia azma ya Serikali ya kuondoa kabisa usafirishaji wa korosho na ufuta ghafi, ambapo Korosho itabanguliwa mkoani Mtwara na mnyororo wote wa thamani wa zao la korosho, ufuta na bidhaa nyingine zinazotokana na maganda yake sambamba na ufuta na kuchakatwa hapa nchini. 

Aidha, Mhe. Rais Samia amewataka wakulima wa korosho kuhakikisha wanakusanya na kuuza korosho yenye ubora ili ziwe na ushindani katika soko la Dunia.

 Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amesema wakulima wakipeleka korosho chafu au zenye grade ya chini wanaharibu sifa ya korosho za Tanzania hivyo suala la kuchambua korosho ni jukumu la mkulima anaelima korosho hiyo.

Vile vile, amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas kusimamia usafirishwaji wa korosho kupitia bandari ya Mtwara ili kudhibiti ubora na kuchochea uchumi wa Mkoa huo.

Pia amepongeza wakulima wa ufuta na zao la mbaazi kwa kuzalisha kwa wingi mazao hayo ambayo kwa msimu wa 2022/2023 wakulima wameuza kwa bei nzuri na yenye kuridhisha.