Skip to main content
Habari na Matukio

SERIKALI YA TANZANIA IMEJIPANGA KUHAKIKISHA UTOSHELEVU WA MBEGU ZA MAZAO

Serikali ya Tanzania inaendelea kutekekeleza mikakati ya kujitosheleza  kwa mbegu za mazao ya kilimo ili  kuihakikishia nchi usalama wa chakula  pamoja na  fursa za kibiashara.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe (Mb) tarehe 24 Mei 2024, alipofungua  Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Mbegu uliofayika jijini Dodoma.

Mhe. Bashe  amewataka  wadau wa tasnia ya mbegu kushirikiana na seeikali katika  uzalishaji wa mbegu  ili kupunguza uagizaji wa mbegu za mazao kutoka nchi za nje ya nchi.

Aidha, Mhe.Bashe ameziagiza taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Kilimo ambazo zinamiliki mashamba ambayo hawayatumii kutoa ardhi hizo kwa sekta binafsi ili waweze kuzitumia kuzalisha mbegu.

Waziri Bashe amewahakikishia wadau mbegu kuwa serikali inaunga mkono uhifadhi na uendelezaji wa mbegu za asili.

Mhe. Bashe amewaasa wazalishaji wa mbegu kuwa na chombo kimoja ambacho kitawaunganisha katika umoja wao ili kurahusisha mawasiliano kati ya yao na serikali.