Skip to main content
Habari na Matukio

SILINDE ASISITIZA UZALENDO PROGRAMU YA BBT

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) amewatia moyo vijana 268 wa programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (Build a Better Tomorrow- BBT) waliopo katika shamba la Chinangali na kuwataka wawe wazalendo ili waweze kutimiza ndoto zao katika Kilimo Biashara.

Amesema leo tarehe 27 Januari 2023 katika shamba la Chinangali, Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma na kusisitiza kuwa  programu ya BBT ni ajenda inayoleta fedha nyingi nchini kusaidia miundombinu na uendeshaji wa shughuli zake za kilimo; huku Mataifa mengine yamekuwa yakijifunza kupitia programu hiyo.  

Akijibu hoja kuhusiana na  hali ya uzalishaji katika shamba la Chinangali, Mhe. Silinde amesema kuwa Serikali ilipanga kuanza uzalishaji wa mboga mboga mara tu wanufaika watakapowasili katika shamba hilo.  Haya hivyo, kutokana na kupitiliza kwa msimu wa uzalishaji wa mazao hayo, vijana hao wataanza na zao la Alizeti wakati wakisubiri msimu mwingine wa kilimo cha mazao ya mboga mboga (horticulture).

Kuhusu vijana zaidi ya 400 wanaotarajiwa kwenda shamba la Ndogowe, Mhe. Silinde amesema barabara zimekuwa zinatengenezwa na TARURA kufuatia miundombinu yake kuharibika na mvua kubwa hali iliyopelekea eneo hilo kushindwa kufikika.