Skip to main content
Habari na Matukio

Silinde atembelea TARI Ukiriguru

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) atembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo (TARI) kilichopo Ukiriguru, mkoani Mwanza tarehe 10 Januari 2023 na kujionea tafiti mbalimbali zinazofanywa na Kituo hicho hususan katika zao la pamba. 

Naibu Waziri Silinde yupo mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi akitokea Mkoa wa Tabora ambapo alitembelea na kukagua kazi mbalimbali zinazofanywa na Bodi ya Tumbaku (TTB) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Tumbaku (TORITA).