Skip to main content
Habari na Matukio

Vijana wa BBT waingia rasmi kwenye shamba la Chinangali

VIJANA waliochaguliwa kwenye Mradi wa  Jenga Kesho iliyobora (BBT) ambao kwa sasa wameshaingia kwenye shamba la Chinangali- Dodoma wameahidi kuzalisha kwa wingi mazao ya mboga na matunda,pamoja na alizeti kwenye shamba hilo kwa ajili ya kuuza ndani na nje ya nchi.

Katika eneo hilo la Chinangali kuna nyumba 33 zilizojengwa kwa ufanisi kwa ajili ya vijana kuishi ambapo ndani yake kuna choo na bafu. Vijana hao kabla ya kuingia shambani kwanza walipata mafunzo kwenye vyuo vya kilisha kisha kuingia  kwenye Mafunzo ya Kijeshi ili kuwajengea uwezo wa kulinda na kuendeleza mali pamoja na kuwa wazalendo JKT.

Wakizungumza na Waandishi wa habari jana kwa nyakati tofauti wakiwa Chinangali, vijana hao mbali na kuahidi kufanya makubwa kwenye kilimo wameishukuru serikali kwa uamuzi wa kuanzisha Mradi huo.

Kijana Rahim Mohamed amesema kuwa kupitia shamba lake la hapo Chinangali atahakikisha analima mazao ya bustani huku akiweka kipaumbele kwenye kulima nyanya, pilipili, mchicha na spinach kwa kuwa mazao hayo yanalimika na kuuzika kwa haraka zaidi.

Amewataka vijana kutoogopa Kilimo isipokuwa wanapaswa hata kwa kutumia ardhi ya nyumbani kwao au kijiji kisha kuweka nguvu kubwa katika kulima mazao kadhaa.