Skip to main content
Habari na Matukio

Wakulima wa Karafuu Mkoa wa Morogoro kunufaika zaidi

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Ally Musa Ally amefanya kikao kazi na wadau wa kilimo cha viungo tarehe 25 Januari 2024 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro na kujadili zao la karafuu. 

Awali, mafunzo ya siku tatu yametolewa kuwajengea uwezo wakulima wenye vitalu vya kuzalisha miche ya karafuu na viungo vingine ambapo wamekuwa wakizalisha miche hiyo bila utaalamu katika eneo la Zigi, Wilayani Muheza.

Kikao kazi kimetoka na maazimio mbalimbali ya kuongeza tija kwenye kilimo cha viungo ikiwemo karafuu; na kugawa miche zaidi ya laki nne kwa wakazi wa Mkoa huo.  Sambamba na hilo, kuwajengea uwezo wakazi wanaokaa katika safu za milima ya Uluguru kupanda miti ya karafuu kwa ajili ya utunzaji wa mazingira. 

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Dkt. Rosalia Rwegasira (Msaidizi wa Uchumi na Uzalishaji) katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Mazao ya Wizara ya Kilimo (Kitengo cha Uzalishaji Mazao), Bi. Beatrice Banzi.