Skip to main content
Habari na Matukio

WALIOHAMA NGORONGORO WATARAJIA KULIMA KISASA

Wananchi  waliohama kwa hiari kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro wanatarajia  kuendesha shughuli za kilimo zinazozingatia mbinu za kisayansi na  kanuni bora za kilimo ili kujihakishia usalama wa chakula na biashara ya mazao ya kilimo.

Wananchi hao watanufaika na mpango huo  kufuatia utekelezaji wa jukumu endelevu la Wizara ya Kilimo la Kutoa Elimu ya Kilimo na Uhakika wa Chakula kwa wananchi hao.

Katika kutekeleza jukumu hilo Wizara ya Kilimo imeshatuma timu ya Wataalamu iliyoongizwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usimamizi na Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Kilimo, Mhandisi Godwin Makori kwa ajili ya  zoezi la uchukuaji wa sampuli za udongo ili kupima afya ya udongo. 

Wananchi watakaonufaika na huduma hiyo ni wa vijiji vya Msomera wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, Saunyi wilaya ya Kilindi mkoani Tanga na Kitwai Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.