Skip to main content
Habari na Matukio

WAZIRI BASHE AKUTANA NA BALOZI WA CANADA

Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe mekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Kyle Nunas.

Waziri Bashe  na Balozi Nunas wamejadiliana namna bora ya kuwekeza katika sekta ya kilimo husan uzalishaji wa ngano ili kupunguza upungufu wa ngano hapa nchini.

Mhe. Bashe amemkaribisha Balozi  Nunas pamoja na sekta binafsi ya Canada kushiriki Mkutato utakaofanyika Septemba 4 hadi 8 jijini Dar esa Salaam, utakaojadili mifumo ya chakula kwa nchi za Afrika(Africa's Food Systems Forum 2023 Summit) ambao pia utakuwa na malengo ya kukuza biashara ya chakula.

Balozi Nunas aliyeambatana  na Kansela Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ubalozi wa Canada,  Helen Fytche  ameipongeza  Serikali ya  Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania   kwa kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo katika mwaka wa fedha 2023/2024 na Programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) yenye lengo la kuwashirikisha Vijana na Wanawake kwenye sekta ya Kilimo.