Skip to main content
Habari na Matukio

WAZIRI BASHE AKUTANA NA WADAU WA PAMBA

 

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb), amefungua na kuongoza Mkutano wa Wadau wa Tasnia ya Pamba tarehe 23 Machi 2024 katika Hoteli ya Morena, jijini Dodoma. 

Mkutano huo umelenga kujadili zao la pamba na kupata mikakati itakayoongeza tija katika uzalishaji na mauzo ya zao hilo.  

Aidha, wadau wamepongeza hatua mbalimbali za Mhe. Rais Dkt. SAMIA Suluhu Hassan katika kukuza Sekta ya Kilimo; ambapo zao la pamba nalo limekuwa sehemu ya utekelezaji wa Wizara ya Kilimo katika kuliinua zao hilo. 

Wakati wa hotuba yake, Waziri Bashe amesema “Serikali ya Awamu ya Sita iko tayari na ina dhamira ya kuimarisha ushirika ili ufanye biashara na kuondokana na tegemezi za tozo za Wakulima. Wito kwa Ushirika kuanzisha miradi ya maendeleo.”

Ameongeza pia kuwa Wizara ya Kilimo itaanza utararibu wa kuhamasisha Mikoa na Wilaya katika kuongeza uzalishaji na tija kwenye zao la pamba kupitia “incentive scheme” ambapo Wilaya au Mikoa itakayoshinda watajengewa vituo vya zana za kilimo ili kurahisisha huduma za uzalishaji wa mazao.  

Waziri Bashe amesema kuwa ni muhimu Mkutano kama huu ufanyike mara mbili kwa mwaka ili kuwa na majadiliano kabla ya msimu wa kulima na baada.  Hivyo, ameomba wadau katika majadiliano kutafakari pia ratiba ya kufanya Mikutano hiyo. 

Waziri Bashe ameambatana na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) na Naibu Katibu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Hussein Mohamed Omar.

Aidha, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kutoka maeneo mablimbali yanayozalisha zao la pamba nchini nao wameshiriki katika Mkutano huo kutoka Simiyu, Mwanza, Tanga, Singida, Geita, Tabora, Mara, Kigoma, Katavi na Kagera.