Skip to main content
Habari na Matukio

WAZIRI BASHE AMUAGIZA MKURUGENZI KUVUNJA MKATABA  

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mdolwa kufuata taratibu za kisheria kuvunja mkataba na Mkandarasi anayejenga mradi wa umwagiliaji katika kata ya Muhukuru wilaya ya Songea mkoni Ruvuma.

Mhe. Bashe ametoa maelekezo hayo baada ya kutembelea ujenzi wa skimu hiyo na kuonesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo.

Waziri Bashe anaendelea na ziara ya kikazi katika mikoa ya Ruvuma, Njombe na Iringa ambapo pamoja na shughuli zingingine atagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya kilimo.

Katika ziara hiyo Mhe. Bashe  atasikiliza na kutatua changamoto na kero mbalimbali za wananchi hususani Wakulima.