Skip to main content
Habari na Matukio

WIZARA YA KILIMO KUENDELE KUWAJENGEA UWEZO WAKUFUNZI WA MATI UKIRIGURU

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Hussein Mohamed Omar amesema Wizara itaendelea kuwajengea uwezo Wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kilimo (MAT) Ukiriguru ili kuweza kuyafikia malengo ya Serikali ya mabadiliko ya utendaji ndani ya Kituo hicho.

Dkt. Hussein Mohamed Omar amesema hayo alipotembelea Chuo Cha MATI Ukiriguru kilichopo jijini Mwanza  ambapo amesema Wizara itatoa fursa za mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu, mabadiliko ya teknolojia ili kuwajengea maarifa zaidi Wakufunzi hao ili kufikisha huduma lengwa kwa wakulima nchini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo, Bw. Frank Mkiramwinyi ameipongeza Serikali kwa kuja na mpango huo kwani utaleta tija ya moja kwa moja kwa Wakulima.