Skip to main content
Habari na Matukio

WIZARA YA KILIMO YASHIRIKI WIKI YA MAZINGIRA

Wizara ya Kilimo kupitia Kitengo cha Mazingira imeshiriki katika Maonesho ya Wiki ya Mazingira Duniani iliyoanza tarehe 29 Mei 2024 na kuhitimishwa tarehe 5 Juni 2024 na Mhe. Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Wananchi walipata fursa ya kupata taarifa za kazi za mazingira, elimu ya kilimo himilivu  na masuala ya mabadiliko ya tabianchi.

Kauli Mbiu ilikuwa: “Urejeshwaji wa Ardhi iliyoharibiwa na Ustahimilivu wa Hali ya Jangwa na Ukame.”