Skip to main content
Habari na Matukio

NAIBU WAZIRI SILINDE AFANYA ZIARA KARATU

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) amefanya ziara ya kikazi Wilaya ya Karatu  na kutembelea Mradi wa Umwagiliaji wa Bonde la Mto Eyasi ambapo kilimo cha vitunguu kinafanyika.

Naibu Waziri Silinde alifanya Mkutano na Wananchi wa eneo hilo na kusikiliza kero zao ikiwemo pendekezo la ujenzi wa skimu za umwagiliaji kujengwa kwa kutumia zege badala ya kutumia mawe ili kuwezesha miradi hiyo kudumu kwa muda mrefu.  Aidha, Mhe. Silinde alielekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kujenga skimu za umwagiliaji kwa kuzingatia maoni ya wananchi na aliwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika na kuwanufaisha katika shughuli zao za uzalishaji wa mazao ya kilimo